SNURA MAJANGA TENA,AFICHUA SIRI NZITO KWA WAKINAMAMA WA NAMNA HII - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Sunday, 21 January 2018

SNURA MAJANGA TENA,AFICHUA SIRI NZITO KWA WAKINAMAMA WA NAMNA HII

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye miondoko ya mduara, Snura Mushi, ameibuka na kudai kuwa mwanamke anayelea watoto mwenyewe ni elimu tosha duniani.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, Snura alisema kuwa, amepata changamoto nyingi sana kwenye kulea watoto wake lakini anashukuru amesimama vyema kama mwanamke shujaa na amejifunza mengi ikiwa ni pamoja na kuwa jasiri ambapo anaweza kusimama popote sasa na kujiamini.
Yaani kulea watoto mwenyewe kama mwanamke ni elimu tosha ya duniani na mimi najivunia hilo sana, mwanzo ilikuwa ni ngumu sana na sisi wanawake tumekuwa tukiwategemea sana wanaume wakiwepo lakini ukiyajaribu maisha ya ulezi peke yako na kuyashinda unajikuta jasiri ambaye unaweza kuingia popote pale,” alisema Snura.

No comments:

Post a Comment