Kenya: Gari la Kanisa lakamatwa likisafirisha Bangi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 16 October 2019

Kenya: Gari la Kanisa lakamatwa likisafirisha Bangi


Polisi waliokuwa wakishika doria kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa hapo jana walipatwa na mshangao baada ya kunasa basi la kanisa likiwa linasafirsha bangi.

Kulingana na ripoti za Polisi, basi hilo lilikuwa limesafirisha waombolezaji kutoka Kilifi kwenda Homa Bay na wakati wa kurudi likapakiwa na bangi hiyo.

Basi la kanisa lilipatikana likisafirisha bangi kwenye barabara ya Nairobi-Mombasa. Tayari dereva wa basi hilo pamoja na watu wengine wawili walitiwa mbaroni ili kusaidia polisi kwenye uchunguzi wa kisa hicho.

OCPD wa Voi Bernastein Shali alisema basi hilo ni la kanisa la PEFA na lilikuwa limebeba mamia ya misokoto ya bangi.

No comments:

Post a Comment