Kipa wa Man United David De Gea hatarini kuikosa mechi ya Liverpool - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 16 October 2019

Kipa wa Man United David De Gea hatarini kuikosa mechi ya Liverpool


Kipa wa Man United David De Gea yupo katika hatihati ya kukosa mechi dhidi ya Liverpool Jumapili hii baada ya kuumia katika majukumu ya timu yake ya Taifa ya Hispania hapo jana.

De Gea alipata maumivu ya nyama za paja katika mechi hiyo ya jana ya kufuzu Euro 2020 ambapo Hispania ilikuwa ikicheza dhidi ya Sweden, mchezo uliisha kwa sare ya 1-1.

Baada ya kupata maumivu hayo De Gea alitolewa katika dakika ya 60 na nafasi yake kuchukuliwa na Kepa Arrizabalaga.

Baada ya mchezo kocha wa Hispania Roberto Moreno alisema kuwa kipa huyo alikuwa anacheza mchezo huo akiwa tayari ana maumivu kabla ya kushindwa kuendelea.

“Alikuwa na maumivu katika misuli ya paja lakini alipokea matibabu wakati wa mapumziko na akataka kuendelea kucheza. Alituahidi (anaweza kucheza), lakini mwishowe akashindwa kuendelea.” amesema.

Kama De Gea atashindwa kukaa langoni siku ya Jumapili Old Trafford dhidi ya vinara wa ligi Liverpool, nafasi yake itachukuliwa na Muargentina Sergio Romero.

No comments:

Post a Comment