Kikao cha Baraza la Madiwani katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa kilichoketi kwa ajenda mahususi ya kumchagua Naibu Meya wa Halmashauri hiyo kimevunjika.Kuvunjika kwa kikao hicho kumetokana na madiwani wa pande mbili za CCM na CHADEMA kushindwa kukubaliana baadhi ya kanuni zilizokuwa zitumike kwenye uchaguzi huo.
Kutokana na hali hiyo ambayo ilisababisha vurugu, ikamlazimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Himid Njovu kuamua kuahirisha kikao mpaka kitakapopangwa tena.
No comments:
Post a Comment