Mbunge awataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 16 October 2019

Mbunge awataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe amewataka wananchi wa Mkoa wa Singida na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha katika daftari la Tamisemi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.

Mattembe ametoa wito huo wakati alipokuwa akiwahamasisha wananchi wa Kata ya Ilongero kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ikiwa imebaki siku moja tu ya kujiandikisha.

Alisema maendeleo  ya nchi yanaanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata, wilaya hadi Taifa hivyo tiketi ya kuweza kuchagua kiongozi mwenye sifa nilazima kwenda kujiandikisha ili kumchagua kiongozi anayefaa.

"Bila ya kujiandikisha haitawezekana kumchagua kiongozi mnaye mtaka hivyo wito wangu kwenu kwa hii siku moja iliyobaki kwa ajili ya kujiandikisha jitokezeni kwa wingi  vinginevyo mtapoteza haki yenu ya kumchagua kiongozi mnaye mtaka” alisema Mattembe.

Aliwataka wananchi hao kujitokeza kujiandikisha bila kujali itikadi ya vyama vyao kwani maendeleo hayana chama yapo kwa ajili ya watu wote.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here