RC Rukwa aagiza Walimu wanaotuhumiwa kuwapa mimba wanafunzi kufikishwa Mahakamani - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 22 October 2019

RC Rukwa aagiza Walimu wanaotuhumiwa kuwapa mimba wanafunzi kufikishwa Mahakamani



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Rukwa kuhakikisha Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya, Dastan Mlelwa anafikishwa Mahakamani kwa madai ya kuwabaka na kuwatia mimba wanafunzi wawili wa kidato cha pili na cha tatu.

Pia, RC Wangabo ameagiza Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mpui iliyopo Halmashauri ya Sumbawanga anayedaiwa kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa kidato cha pili shule hapo na mwanafunzi huyo kuhamishiwa Shule ya Sekondari ya Mazwi Manispaa ya Sumbawanga, akamatwe na afikishwe Mahakamani.

Hii imekuja baada ya Rais Magufuli kufanya ziara mkoani Rukwa na kushangazwa na wanaume kutochukuliwa hatua baada ya kuwapa mimba wanafunzi 229 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Rais Magufuli alisema mkoa wa Rukwa ndio unaongoza kwa wanafunzi kupata mimba na kuwataka wanafunzi kuacha kiherehere na kujikita kwenye masomo kwani hayo watayakuta tu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here