Taarifa kuhusu uzinduzi wa huduma ya tiba ya Dialysis Hospitali Kuu ya Jeshi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 22 October 2019

Taarifa kuhusu uzinduzi wa huduma ya tiba ya Dialysis Hospitali Kuu ya Jeshi



Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika jitihada za kuboresha huduma ya Afya linatarajia kuzindua Idara mpya ya huduma ya Tiba ya Dialysis katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo.

Shughuli za uzinduzi huo zinatarajia kufanyika kesho Jumatano tarehe 23 Oktoba, 2019 kwenye Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo iliyopo Jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili na nusu (2:30) asubuhi.

Mgeni rasmi katika shughuli hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

JWTZ limealika vyombo vya Habari kwenye hafla hiyo muhimu ili kuuhabarisha umma juu ya huduma hiyo kupatikana Jeshini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here