Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na wale wanaofanya kazi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo wameaswa kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na uadilifu kwa kuwa hiyo ndiyo silaha pekee kwa Mtumishi wa Umma.Haya yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare alipokuwa anazungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mwendelezo wake wa kujitambulisha kwa kila Halmashauri na kuzungumza na watumishi ili kusikiliza changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.
Amewataka watumishi hao kusimama imara katika kufanya kazi na kutumia weledi wao kwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kwamba uadilifu ndiyo silaha muhim katika kufanya kazi ya Umma.
“Uadilifu katika kufanya kazi ni kitu kizuri sana, msishangilie kwa sababu mmeona wengine na kweli walimopita mmeona kilichotokea, sasa aje hapa akute tuko wamoja na tunachapa kazi” alisema Sanare.
Hata hivyo, Sanare anaendelea kuwakumbusha watumishi wote wa Umma kutumia vema rasilimali za Serikali zilizopo iwe fedha za kutoka Serikali Kuu ama fedha zinazokusanywa na Halmashauri.
No comments:
Post a Comment