Waziri Biteko ashiriki kujadili changamoto za barabara - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 16 October 2019

Waziri Biteko ashiriki kujadili changamoto za barabara


Waziri wa Madini Doto Biteko ameshiriki katika Kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ili kujadili changamoto za barabara mkoani hamo. 

Kikao hicho kiliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapindizi wakiwemo Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Geita akiwemo Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini Doto Biteko, Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma, Mbunge wa Mbogwe Augustino Masele, Mbunge wa Busanda Lolesia Bukwimba, Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema Pendo Peneza.

Vingozi wengine walioshiriki ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mjini Josephat Maganga, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Mkumba, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe. Martha Mkupasi, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Geita Alhaji Said Kalidushi pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali.

Aidha Waziri Biteko amewapongeza viongozi wa TANROADS na TARURA kwa kazi nzuri wayoifanya katika Mkoa wa Geita kwa kuhakikisha kuwa barabara zinatengenezwa kwa kiwango kizuri na kumalizika kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Biteko amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri katika kuhakisha barabara za Mkoa wa Geita zinakamilika kwa muda uliopangwa na zinakuwa kwenye viwango vinavyotakiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here