Kesi ndogo kina Mbowe yaendelea - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Wednesday, 10 November 2021

Kesi ndogo kina Mbowe yaendelea

 


Kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu inatarajia kuendelea kuunguruma leo Jumatano katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.


Kesi hii ndogo inatokana na pingamizi la mawakili wa utetezi kupinga kupokewa maelezo ya onyo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa wa tatu katika kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi.


Mawakili hao walicharuka baada ya shahidi wa nane wa Jamhuri kuiomba mahakama iyapokee kama kama sehemu ya ushahidi.


Shahidi huyo, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru (OC-CID), mkpani Arusha, Mrakibu wa Polisi (SP) Jumanne Malangahe aliieleza mahakaka hiyo kuwa ndiye aliyeandika maelezo ya Mshtakiwa wa tatu, Mohamed Abdillahi Ling’wenya.


No comments:

Post a Comment