Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 11.11.2021 - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 11 November 2021

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 11.11.2021

 


Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anataka kuongeza mkataba wake na klabu ya Manchester United , lakini mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 anataka kumpiku Christiano Ronaldo ili kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi katika ligi ya Premia. (L'Equipe, via Metro)


Barcelona inajiandaa kuimarisha safu yake ya mashambulizi mwezi Januari kwa kumsajili mshambuliaji wa England Raheem Sterling , 26 mshambuliaji wa Man United na raia wa Uruguay Edinson Cavani ,34 na mchezaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 25 Timo Werner wa Chelsea, wote wakifikiriwa.


Mshindi mara sita wa taji la Ballon d'Or Lionel Messi , 34, huenda akarudi Barcelona licha ya mshambuliaji huyo Kuondoka katika ligi hiyo na kujiunga na mabingwa wa Ufaransa PSG katika kipindi cha miezi mitatu iliopita. (Daily Star)


Aston Villa itawalipa Rangers takriban £3m kama fidia iwapo Steven Gerrard atakuwa meneja wao mpya (Times)


Newcastle ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot ,26, katika dirisha la mwezi Januari (Calciomercato, via Mirror)


Lakini Newcastle itaona vigumu kumnunua ama hata kuwanunua kwa mkopo kutoka kwa ligi ya Uingereza mwezi Januari kwasababu klabu kuu hazitaki kufanya biashara nao. (Telegraph)


Liverpool inajiandaa kuwanunua wachezaji 3 katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari ili kuchukua mahala pao wachezaji Mohamed Salah, Sadio Mane na Naby Keita wakati watatu hao watakapojiunga na timu zao za kitaifa kwa kombe la bara Afrika , huku kiungo wa Inter Milan `na raia wa Croatia Marcelo Brozovic ,28 akifikiriwa pia. (Daily Star)


Agenti maarufu Jorge Mendes anajaribu kumuunganisha kiungo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 19 Fabio Carvalho na klabu ya Liverpool (Daily Mail)


Mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic bado analengwa na Juventus , licha ya kuvutia hamu kutoka kwa klabu kuu za ligi ya Premia kwa raia huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 21.(Tuttosport - in Italian)



Maskauti wa klabu ya Ujerumani ya Bayern munich wamekuwa wakimchunguza mshambuliaji wa West Brom mwenye umri wa miaka 17 Reyes Cleary ambaye amefunga magoli 12 msimu huu. (Daily Mail)


Beki wa Denmark Andreas Christensen 25 ameambia mashabiki wa Chelsea kutojali kuhusu hatma yake licha ya kandarasi yake kuisha msimu ujao wa joto.. (Standard)


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here