Waziri wa kigeni wa UAE akutana na rais wa Syria - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 10 November 2021

Waziri wa kigeni wa UAE akutana na rais wa Syria

 


Waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu amekutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad. Ziara hiyo ya Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan inatoa ishara kuwa ulimwengu wa Kiarabu uko tayari kurudisha tena uhusiano na kiongozi huyo aliyesusiwa kwa muda mrefu tangu kuanza vita nchini mwake mnamo mwaka 2011. 


Marekani ambayo ni mshirika wa karibu wa Umoja wa Falme za Kiarabu imeikosoa ziara hiyo, na kusema haitounga mkono hatua zozote za kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia na Assad. 


Mkutano huo unatajwa kuwa na manufaa kwa mataifa yote mawili. Serikali ya Syria inahitaji kurudisha uhusiano mzuri na mataifa ya Kiarabu yenye utajiri wa mafuta, kwani inakabiliwa na kibarua cha kuijenga tena nchini hiyo. 


Na Umoja wa Falme za Kiarabu unanufaika kwa kuajiri maelfu ya raia wa Syria wanaoishi nchini humo na kutuma pesa nyumbani kuzisaidia familia zao.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here