Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua upanuzi wa Hospitali ya Tumbi.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maagizo kwa uongozi
wa mkoa wa Pwani na watendaji wakuu wa Shirika la Elimu Kibaha ambao
Hospitali ya Tumbi ipo chini yao.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ramani ya upanuzi wa jengo la hospitali ya Tumbi Kibaha.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akimsalimiana na mgonjwa
ambaye ni mlemavu wa viungo katika Hospitali ya Tumbi.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa
mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Tumbi iliyopo mkoani Pwani.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi ameutaka Uongozi wa Shirika la
Elimu Kibaha na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kukaa pamoja na
kufanya Maamuzi ya haraka ndani ya wiki moja wafikie makubaliano ya
uendelezaji wa ujenzi wa jengo jipya la upanuzi wa hospital ya Tumbi
ambayo ni hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani.
Jafo
ameoneshwa kukerwa na ugoigoi wa kufanya maamuzi unaoendelea licha ya
serikali kupeleka fedha kiasi cha sh.milioni 685 katika mwaka wa fedha
2016/2017 lakini mpaka sasa wameshindwa kufanya Maamuzi.
Naibu
Waziri Jafo amesema kitendo hicho kinachelewesha kuwapatia huduma bora
wananchi.Kutokana na hali hiyo, Jafo amewaonya watendaji hao na kuagiza
hadi wiki ijayo wawe wamekamilisha mkataba wa makubaliano na ujenzi
uanze mara moja.
No comments:
Post a Comment