anzania kuwapatia mafunzo Wanawake wajasiliamali kutoka Somalia na Sudan kusini - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Monday, 2 October 2017

anzania kuwapatia mafunzo Wanawake wajasiliamali kutoka Somalia na Sudan kusini


Chama cha Wafanyabiashara Wanawake nchini TWCC kimekuwa mwenyeji wa wanawake wajasiriamali kutoka nchi za Somalia, Chad na Sudan Kusini, ambao wapo nchini kwa kozi ya mwezi mmoja, kwa ajili ya kujifunza shughuli mbali mbali za ujasiriamali

 na uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Mwenyekiti wa TWCC Bi. Jacqueline Maleko amesema kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo nchini SIDO, wamewapatia wanawake hao mafunzo katika fani mbali mbali za ujasiriamali ikiwa ni pamoja na kutembelea Chuo cha Uvuvi Mbegani ambako wamepatiwa mafunzo ya uokaji wa samaki wabichi.

Kwa upande wao, akina mama hao wameishukuru Benki ya Dunia iliyofadhili mafunzo yao kutokana na umuhimu wake katika nchi zao ambazo kwa sasa zina machafuko ya kisiasa ambayo yamekuwa yakiwazuia wanawake kupatya ujuzi wa ujasiriamali

No comments:

Post a Comment