Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqqaro amewataka wananchi wa wilaya
ya Arusha Mjini Kuchangamkia zoezi la Uandikishwaji Vitambulisho vya
Taifa (NIDA) ambalo linaendelea katika kata tatu za Wilaya hiyo.
Akizungumza
katika kipindi cha Goodmorning Tanzania kinachorushwa na kituo cha
Matangazo cha Redio cha Redio 5 Arusha Daqqaro, amesema kuwa zoezi hili
lina manufaa makubwa kwa wananchi na watanzania kwa ujumla lakini pia
vitambulisho hivyo vitawawezesha watanzania kutambulika kila mahala,
pamoja na raia wa kigeni kufanya shughuli zao bila usumbufu ikiwa ni
pamoja serikali kuwa na taarifa sahihi za wananchi.
Aidha
amesema kuwa wananchi wasisubiri mpaka zoezi hilo kufikia tamati ndio
kujitokeza Kwa wingi kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha msongamano
na usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Naomba
niwafahamishe na kutoa rai kwa wananchi wangu wajitokeze kwa wingi
katika zoezi hili na wasisibirie siku kubaki chache ndio wajitokeze kwa
kuwa kunapelekea usumbufu mkubwa sana hivyo,zoezi hili pia litakuwa na
manufaa makubwa kwa wananchi”alisema fabian
Pia
ametaka kila mwananchi kushiriki zoezi hilo na kutolihusisha na masuala
ya kisiasa kutokana na umuhimu wake,kwa kuwa lengo ni kutambua na
kusajili na kutoa vitambulisho vya taifa.

Afisa
kutoka mamlaka hiyo wilaya ya Arusha Mjini Juliette Raymond Amesema
lengo la zoezi hilo ni kuwezesha serikali kutambua wananchi wake wapo
wapi na wanafanya nini ilimradi anaishi ndani ya mipaka ya Tanzania
,hivyo zoezi hilo ni lazima kwa kila mtu kwa Mujibu wa sheria.

Kwa
wilaya ya Arusha Mjini zoezi hilo linaendelea katika kata ya
Sombetini,Sekei na Themi ambapo zoezi hilo linafnyika katika Halmashauri
ya Jiji la Arusha katika kata ya Sekei,Themi katika viwanja vya nane
nane na Sombetini Ofisi za Mtendaji kata eneo la Mbauda Sokoni.



No comments:
Post a Comment