Akizungumza na waandishi wa habari
Mratibu wa Tamasha hilo Zamaradi Nzowa amesema kuwa tamasha hilo
litasaidia kukuza taaluma ya filamu na kuongeza ubunifu na kutambua
ubora wa ufanisi katika tasnia ya filamu.
Amesema kuwa tamasha hilo pia
litaonyesha filamu zaidi ya 150 na kutoa tuzo kwa washiriki mbalimbali
katika taaluma tofauti za tasnia hiyo.
Naye Mkurugenzi wa tamasha hilo Jacob
Joseph amesema kuwa kupitia tamasha hilo wamebuni mbinu maalum ili
kuwafikia wadau wa tasnia duniani kote.
Amesema ili kuhakikisha kuwa wanawafikia
wadau wote Afrika mashariki watakuwa na vituo maalum mikoani na katika
nchi za Afrika mashariki ili kueneza, kuhamasisha na kupokea filamu
zitakazowasilishwa katika mashindano.
Amesema vituo hivyo vitakuwa katika
Mikoa ya Morogoro, Zanzibar, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na
Mtwara lakini pia Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura na Goma.
Kwa upande wake balozi wa tamasha hilo
Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amesema kuwa uzuri wa tamasha hilo
ni kuwa filamu zote zinaweza kushindanishwa na hakuna upendeleo wowote.
Amesema jopo la waamuzi ni la kimataifa
na litahakikisha haki inatendeka na uwepo wa jopo hilo la watu 25
linatokana na wadau tofauti wa tasnia.
Hata hivyo katika tamasha hilo
kutatolewa tuzo ambazo zitakuwa na fedha itakayofikia milioni 5 kwa
filamu bora na filamu zitakazo shindanishwa ni Bongo movie, filamu fupi
na filamu za makala.
No comments:
Post a Comment