Wafanyakazi wa
Benki ya NBC Tawi la Samora wakipozi kwa picha ya pamoja wakiwa katika
umbo la moyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu kwa wateja
wao kipindi hii benki yao ikiendelea kuadhimisha mwezi wa huduma kwa
wateja.
Mteja wa Benki ya
NBC, Neema Xibona (kulia) akionyesha furaha mbele ya wafanyakazi wa
benki hiyo Tawi la Samora, Dar es salaam ambapo sasa NBC inaendelea
kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Wafanyakazi hao wanatumia muda
wao kuwa karibu na wateja kusikiliza maoni yao kuhusu huduma na
changamoto wazipatazo na kuzitafutia ufumbuzi.
Meneja wa Benki ya
NBC Tawi la Mbagala, Sady Mwang’onda (kulia), akizungumza na mmoja wa
wateja, Elias Kaaya alipofika katika tawi lake kupata huduma.
Meneja wa Benki ya
NBC Tawi la Kichwele, Frank Mwanga (kushoto), akisalimiana na mmoja wa
wateja waliofika katika tawi hilo jijini Dar es Salaam kupata huduma
ambapo pia alipata nafasi ya kutoa maoni yake kuhusu huduma zinazotolewa
na benki hiyo.
Wafanyakazi wa
Benki ya NBC Tawi la Chang’ombe wakirusha maputo pamoja na wateja wao
kusherehekea mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.
Meneja wa NBC Tawi
la Samora, Faustina Maeda, akimkaribisha Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC,
James Kinyanyi (kulia) alipotembelea katika tawi hilo kuangalia ubora
wa huduma zinazotolewa kwa wateja na pia alipata nafasi ya kuzungumza na
baadhi ya wateja.
No comments:
Post a Comment