.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar),
Salum Mwalimu amesema kwamba matukio yanayoendelea hayawezi kuwaziba
midomo au kusimamisha kazi zao bali yanazidi kuwaimarisha zaidi kisiasa.
Leo wakizungumza kwenye makao makuu ya
Chama jijini Dar es salaam mbele ya wanahabari, Mwalimu amekanusha
tetesi za kwamba chama kimefungwa mdomo na kubweteka tangu tukio la
kushambuliwa kwa Mwanasheria wao Mkuu wa chama na Mbunge wa Singida
Mashariki Tundu Lissu.
Mwalimu amesema kwamba tukio la
kushambuliwa kwa kiongozi wao hakujafanya chama hicho kushindwa
kuendelea na shughuli za chama na badala yake wanaendelea kuimarisha
chama kupitia kampeni ya Chadema ni Msingi zinazoendeshwa nchi nzima
pamoja na kuweka mikakati ya kushinda kwenye uchaguzi mdogo.
"Tupo kwenye vikao vizito vya
kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye uchaguzi mdogo uliotangazwa. Tukio
hili la Lissu halijafanya shughuli za chama zisimame, Shughuli
zinaendelea kama kawaida. Mikoani na makao makuu ya chama mambo yetu
yanaenda kama awali. Tuna kampeni kubwa inaendelea nchi nzima inaitwa
'Chadema ni msingi'.
Hatuwezi kusimama na kwanini tusimame
tunazidi kuimarika kila siku. Kwa yanayoendelea wapo wanaodhani
yatatuziba midomo lakini ndo yanatupa hamasa zaidi ya kuendelea
kuwatetea" Mwalimu.
Ameongeza kwamba "Napenda kuwahakikishia
Watanzania hatujatetereka kwa yanayoendelea tupo imara, chama hiki ni
chao kitaendelea kuwa kipaza sauti zao".
Aidha Mwalimu amesema kuhusu afya ya Mh. Lissu siku chache zijazo watatoa taarifa kuhusu maendeleo yake.
No comments:
Post a Comment