
Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es
salaam limempa siku 3 tu Sheikh Issa Ponda, ili kujisalimisha na
kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, na iwapo hatafanya hivyo
watamchukulia sheria stahiki.
Tarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari, na kusema kwamba ndani ya siku hizo 3 lazima awe amekwenda
kujisalimisha, la sivyo hatakuwa salama.
“Ametenda makosa ya jinai kama
uchochezi, lakini pia amekuwa anatoa lugha ambazo ni za kejeli, dhidi ya
serikali, anatufutwa na kama unamjua mwambie ajisalimishe ili tuweze
kumhoji, kukimbia hakutomsaidia, tukiona kuna kosa la jinai tutampeleka
mahakamani kama hana tutamwachia, mimi nampa siku tatu lakini akija leo
ni nzuri zaidi, nampa siku 3 ajitokeze mwenyewe aweze kuhojiwa,
vinginevyo hatakuwa salama”, amesema Kamanda Mambosasa.
Hapo jana Jeshi la polisi lilivamia
mkutano wa Sheikh Ponda aliokuwa nafanya na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam, na kufanikiwa kukamata baadhi ya watu wakiwemo waandishi
wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment