
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kutoa uamuzi wa ama kupokea au
kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Se...
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama
kutoa uamuzi wa ama kupokea au kutopokea kielelezo cha hati ya
ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu katika kesi ya kutumia dawa za
kulevya kwa sababu Hakimu hajamaliza kuandaa uamuzi huo.
Uamuzi huo ulitarajiwa utolewe leo
October 4, 2017 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini amesema bado
hajamaliza kuandaa uamuzi huo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi November
1, 2017.
Awali, Wakili wa Wema, Peter Kibatala aliiomba Mahakama isipokee hati hiyo kwa kuwa haikukidhi vigezo.
Mbali ya Wema, washtakiwa wengine ni
Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambao wanakabiliwa na mashtaka mawili
ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za
kulevya.
No comments:
Post a Comment