KUKAMILIKA
kwa Mradi wa ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 220kV, na
usambazaji umeme vijijini kutoka Makambako-Songea kupitia Njombe,
unatarajiwa kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa
wananchi wa mijini na vijiji vipatavyo 191, Meneja wa Mradi huo
Mhandisi Didas Liyamuya,(pichani juu), amesema leo Jumanne Oktoba 10,
2017 wakati wa ziara ya Wahariri wa vyombo vya habari nchini.
Sambamba
na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pia utahusisha upanuzi wa kituo
cha kupoza umeme cha Makambako cha msongo wa umeme wa kilovolti
220/132/33Kv, na ujenzi wa vituo vingine vipya viwili, vya Madaba na
Songea vya msongo umeme wa kilovolti 220/33kV, halikadhalika ujenzi wa
mfumo wa usambazaji umeme wa msongo wa kilovoti 33 pamoja na kuunganisha
wateja 22,700, katika mikoa hiyo alisema Mhandisi Liyamuya.
Akifafanua
zaidi, katika mkoa wa Njombe, umeme utasambazwa katika maeneo ya
Makambako na viunga vyake, Njombe yenyewe, na Ludewa, wakati mkoa wa
Ruvuma umeme utasambazwa katika mji wa Songea na vijiji vilivyo katika
wilaya ya Mbinga, Namtumbo na Madaba, na kuongeza kuwa umeme utakuwa wa
msongo wa kilovolti 33 pamoja na ujenzi wa mawasiliano “OPGW”.
“Lengo
la mradi huu ambao unafadhiliwa na Serikali ya Swedena kupitia Shirika
lake la Misaada ya Kimaendeleo SIDA, Serikali ya Tanzania na Shirika la
Umeme Nchini, TANESCO, ni kuboresha hali ya upatikanaji umeme katika
maeneo ya uzalishaji na majumbani.” Alifafanua.
Wahariri
hao walipata fursa ya kutembelea eneo la upanuzi wa kituo cha Makambako
ambapo walishuhudia kazi ya kujenga misingi ya mitambo ikiwemo Slope
protection. Pia walijionea kazi ya kufunga transfoma kwenye maeneo
kadhaa ya Makambako ikiwemo eneo la Lyamkena.Mhandisi Liyamuya
alibainisha kuwa awamu ya kwanza ya mradi wa kusambaza umeme utakamilika
Desemba 2017 wakati awamu ya pili utakamilika Novemba 2018.
“Hadi
leo hii Oktoba 10, 2017, mradi umekamilika kwa asilimia 63 kwa upande wa
mkoa wa Ruvuma na asilimia 39.5 kwa upande wa mkoa wa Njombe na kazi
kubwa iliyofanyika ni ubainishaji wa maeneo ya kupitisha laini (njia ya
umeme), ubunifu wa jinsi muundo wa njia hiyo utakavyokuwa, ufyekaji wa
njia za kupitisha laini, ununuzi wa vifaa pamoja na kusimamisha nguzo za
msongo wa 33kV na 400V na kusambaza nyaya, na usimikaji wa Transofa.”
Alisema.
Hata
hivyo Mhandisi Lyamuya alieleza masikitiko yake kwa baadhi ya watu
kuchoma moto ovyo misitu ambapo baadhi ya nguzo zilizosimikwa katika
kipindi hiki cha mradi zimeungua.
“Nitoe
rai kwa watanzania wenzangu, Serikali inafanya juhudi kubwa
kuwafikishia huduma hii muhimu ya umeme, na mfahamu kwamba fedha za
walipa kodi wa Tanzania Shilingi Bilioni 7 zilitolewa kama fidia, iweje
leo tuanze kufanya uharibifu huo.?” Alihoji, na kutaka vimgozi wa
serikali kwenye maeneo yote ya mradi kuwahamasisha wananchi kutunza
miundombinu hiyo ambayo inaligharimu taifa fedha nyingi.
Mmoja
wa wakazi wa kitongoji cha Lyamkena, mji wa Makambako mkoani Njombe,
ambaye ni mteja mpya wa TANESCO, Bw.Thomas Kiwale, (kulia), akihakikiwa
wakati wa zoezi la kuwahakiki wateja walioomba kuunganishiwa umeme
kwenye eneo hilo, na afisa wa TANESCO, Bi.Atuokoe Mhingi, Oktoba 10,
2017
Wahariri
na mafundi wa TANESCO, wakipita chini ya moja ya transofa zinazoednelea
kufungwa kwenye mji wa Makambako Oktoba 10, 2017.
Baadhi
ya wahariri wakisikiliza maelzo yaliyokuwa yakitolewa na Mhandisi
Liyamuya(hayupo pichani), kuhusu utekeelzaji wa mradi huo walipotembelea
eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza na kusafirisha umeme wa 220kV cha
Makambako.
Baadhi
ya wahariri na mafundi wa TANESCO, wakisikiliza maelzo yaliyokuwa
yakitolewa na Mhandisi Liyamuya(hayupo pichani), kuhusu utekeelzaji wa
mradi huo walipotembelea eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza na
kusafirisha umeme wa 220kV cha Makambako.

Kaimu
Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bil Leila Muhaji, akifafanua baadhi ya mambo
ambapo alisema, ili kujenga uhusiano mwema na wananchi walio jirani na
eneo la Mradi, wateja watatozwa kiasi cha shilingi 27,000 tu kwa kazi
hiyo katika kipindi hiki cha utekelezaji wa mradi, na hivyo kuwataka
wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme kwa faida ya taifa na wao
wenyewe.
Bi.Atuokoe
Mhingi,kutoka TANESCO, akiendelea na zoezi la kuwahakiki wateja
walioomba kuunganishiwa umeme kwenye eneo la Lyamkena, Makambako Oktoka
10, 2017.
Moja ya minara ya kusafirisha umeme wa 220kV. ambao tayari umejengwa nje kidogo ya mji wa Makambako.
Moja ya minara ya kusafirisha umeme wa 220kV. ambao tayari umejengwa nje kidogo ya mji wa Makambako.
Mhariri wa Mwananchi Online Digital, Peter Nyanje, (kushoto) na Mhariri wa gazeti ka Majira, Bw. Mwafisi wakifurahia jambo.
Mhariri
wa gazeti la Nipashe, Bw. Joseph Mwendapole, (kulia), akionyeshwa moja
ya minara ya kupitisha umeme wa 220kV nje kidogo ya Makambako.
Kazi ya ujenzi wa msingi wa kufunga mitambo kwenye eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza umeme wa 220kV Makambako ikiendelea.
Kaimu
Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (kulia) na Afisa Uhusiano
wa Shirika hilo, Bi. Grace Kisyombe wakijadiliana jambo.
Meneja
Mradi wa ujezni wa njia ya kusafirisha umeme kutoka kampuni ya
Isolux,Bw.Elmensour,(kulia), akielezea jinsi kazi hiyo inavyoendelea














No comments:
Post a Comment