Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula
akiwashukuru kampuni ya FT Trucks & Equipments kwa kuipatia udhamini
kwa timu ya mkoani kwake Mwanza pamoja na basi sambamba na yeye kuwa
mlezi wa timu hiyo leo Jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula na
Mbunge wa Ilemela, ameishukuru Kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa
kutimiza ahadi yao kwa Mbao kwa kukabidhi gari yenye thamani ya milioni
70 na tayari wakiwa wamelipia gharama zote za ushuru na kufikia jumla
ya milioni 100.
Mabula
amesema kuwa baada ya kuingia mkataba na kampuni hiyo wameanzisha
kampeni ya ubingwa ili kulitoa taji kwa timu za Mkoa wa Dar es Salaam na
wanaweza kufanikiwa kwa hilo kama wadhamini watajitokeza kwa wingi kwa
timu za mikoani.
Mbao FC ya Mwanza imekabidhiwa basi lenye thamani ya Sh70 milioni kwa ajili ya wachezaji.Basi
hilo wamekabidhiwa leo Jumatano na wadhamini wao Kampuni ya GF Trucks
& Equipments katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Vingunguti,
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Alijawad Karmali alisema basi
hilo ni sehemu ya mkataba ambao waliingia na Mbao miezi miwili
iliyopita na wameweza kutimiza ahadi hiyo na wanaimani kuwa watalitunza
katika kipinci chote..
Mwenyekiti
wa Mbao FC, Solly Njashi amewashukuru Kampuni ya GF Trucks &
Equipments kwa udhamini huo mkubwa waliouweka kwani mpaka basi hilo
wanalipokea katika mikono yao limezidi thamani ya Sh70 milioni na
litakuwa msaada mkubwa sana kwa timu yao kuhusiana na masuala ya usafiri
na pia mpaka sasa udhamini wao umeshazidi milioni 140
Mbao
inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi
sita, huku Simba ikiwa kileleni na pointi 12 ikifuatiwa na Yanga ambayo
ndiyo mabingwa watetezi wakiwa na tofauti na mabao ya kufunga na
kufungwa.
Ofisa
Masoko wa Kampuni ya GF Trucks Equipment, Kulwa Bundala akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na kuwakabidhi gari lenye thamani ya
milioni 70 kwa timu ya Mbao ikiwa ni moja ya makubaliano yaliyopo katika
udhamini wao wa mwaka mmoja kwa timu hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula pamoja na
Mkurugenzi wa GF Trucks & Equipments Alijawad Karmal
(kulia) na mwenyekiti wa timu ya Mbao Solly Zephania Njashi wakikata
keki.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula
akikata utepe katika gari ya waliokabidhiwa Mbao na kampuni ya GF
Trucks & Equipments lenye thamani ya milioni 70 ikiwa ni katika
makubaliano ya mkataba walioingia miezi mitatu iliyopita, juu ni
Mkurugenzi wa GF Trucks & Equipmens Alijawad Karmal akimkabidhi
mfano wa funguo ya gari mwenyekiti wa timu ya Mbao Solly Zephania Njashi
akishuhudiwa na viongozi wengine wa Mbao Fc pamoja na wengine kutoka GF
Trucks & Equipments.
Muonekano wa basi walilokabidhiwa timu ya mpira wa miguu Mbao Fc
ya Jijini Mwanza na kampuni ya GFTrucks & Equipments leo mbele ya
Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula
ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela na mlezi wa timu hiyo.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na
Makazi Angelina Mabula na viongozi wa timu ya Mbao Fc na wafanyakazi
kutoka kampuni ya GF Trucks & leo jijini Dar es salaam wakati wa
makabidhiano ya basi lenye thamani ya milioni 70
No comments:
Post a Comment