Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora ambaye sasa amekuwa Waziri wa Madini Angelah Kairuki
(kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora
George Mkuchika wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya ofisi leo jijini
Dar es Salaam leo. Wengine ni watumishi wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
George Mkuchika, akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari leo
Jijini Dar es Salaam katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa
Waziri wa wizara hiyo Angellah Kairuki ambaye sasa amekuwa Waziri wa
Madini
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora ambaye sasa amekuwa Waziri wa Madini Angelah Kairuki
akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari katika hafla ya kumkabidhi
ofisi mrithi wake Waziri George Mkuchika leo Jijini Dar es Salaam .
Aliyekuwa
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angelah Kairuki akimkabidhi nyaraka za ofisi Waziri aliyeteuliwa
kuongoza Wizara hiyo George Mkuchika katika hafla iliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angelah Kairuki akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari
katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na waziri aliyeteuliwa kuongoza
wizara hiyo George Mkuchika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
George Mkuchika amesema kuwa atashughulikia suala la rushwa pamoja na
udanganyifu wa umri unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma hapa
nchini.
Mkuchika
aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika mkabidhiano ya Ofisi na
aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo ambaye kwa sasa ni Waziri wa Madini,
Angellah Kairuki katika ukumbi wa wizara hiyo.“Tutaongeza kasi ya kurejesha nidhamu, maadili na mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini,” alifafanua waziri Mkuchika
Katika
hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.
Laurean Ndumbaro pamoja na watumishi wa wizara hiyo, Waziri Mkuchika
alisema kuwa atahakikisha anashughulikia suala la watumishi kupandishwa
madaraja pamoja na kuongezewa mishahara baada ya kukamilika zoezi la
ukaguzi la watumishi hewa.
Aidha
alisema kuwa suala la rushwa linatakiwa kujengewa msingi kutoka ngazi ya
chini, hivyo ataongea na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako ili kuweka somo la rushwa katika mitaala ya elimu hapa
nchini kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu.
“Ukienda
katika nchi ambazo zimefanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa, mfano
Norway, Sweden, pamoja na mataifa ya Scandinavia utakuta wamefanikiwa
kwasababu wananchi wote wamepewa elimu dhidi ya rushwa na wanafahamu
kwamba rushwa ni adui wa haki, lakini tujiulize watanzania wangapi
wanajua kuwa rushwa ni adui wa haki, ni wachache tu,” alisema Waziri
Mkuchika.
Aliongeza
kuwa, makongamano, semina pamoja na mikutano inayofanya na watumishi wa
umma kwa wananchi inapaswa ishirikishe Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
Rushwa (TAKUKURU) ili kutoa elimu juu ya rushwa na kujenga uelewa kwa
wananchi kwani itasaidia sana kumaliza tatizo la rushwa hapa nchini.
Waziri
Mkuchika alimpongeza mtangulizi wake na kuahidi kuendeleza jitihada
alizokuwa akiendelea nazo ikiwemo kuondoa watumishi hewa, vyeti feki,
wanaoghushi umri pamoja na uzembe wa wafanyakazi katika ofisi za umma
hususani katika Halmashauri.
Kwa
upande wake Waziri Kairuki, aliwapongeza watumishi wa Idara, Wakala wa
Serikali, Taasisi pamoja na Wizara hiyo kwa ujumla kwa ushirikiano na
ushauri walioutoa kwa muda aliofanya nao kazi takribani miaka miwili kwa
kuimarisha nidhamu, maadili na kuondoa watumishi hewa katika ofisi za
umma.
“Tumeweza
kurejesha kwa kiasi kikubwa nidhamu katika utumishi wa umma, tumeweza
kwa kiasi kikubwa kuanza kujenga misingi ya kuelekea katika kuboresha
masilahi ya watumishi umma maana ilikuwa ni lazima tuanze kusafisha
kwanza lakini pia tumeweza kuondoa watumishi hewa, pamoja na kuondoa
watu ambao hawakuwa na sifa stahiki katika utumishi wa umma,” alifafanua
Waziri Kairuki.
Waziri
Mkuchika aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kufuatia mabadiliko yaliyofanywa katika
baraza la mawaziri na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli, ambapo aliyekuwa anaongoza wizara hiyo Angelah Kairuki
aliteuliwa kuwa waziri wa madini.
No comments:
Post a Comment