BARAZA
la Vyama vya hiari na Maendeleo ya Jamii (TACOSODE) limesema wananchi
wamekuwa na uelewa kuhamasisha bajeti kuwa na kipaumbele kwa changamoto
zinazowakabili.
Hayo
ameyasema Mkurugenzi wa Miradi wa Tacosode, Theofrida Kapinga wakati
akizungumza semina ya kujadilia jinsi gani ya kutatua changamoto
zinazoikumba sekta ya afya iliyofanyika katika ukumbu wa valentine
Manispaa ya Iringa.
“Unajua
zamani wananchi hata viongozi wa sekta ya afya walikuwa wagumu kuelezea
changamoto zinazowakabili lakini saizi wananchi na viongozi wamekuwa na
elimu ya kutosha juu ya kueleza changamoto zilizopo katika sekta hiyo
ndio maana vitu vingi vinaibuka muda huu” alisema Kapinga
Kapinga
alisema licha ya serikali kufanya juhudi kutatua changamoto ili kuto
huduma ya afya bora lakini bado sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na
changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha upatikanaji wa huduma bora za
afya kwa wananchi.
“Ukiangalia
tafiti nyingi zinaonyesha kuwa serikali imekuwa ikishindwa kuongeza
bajeti ya sekta ya afya ili kufikia asilimia 15 ya bajeti yote ya
serikali kwa kuzingatia azimio la Abuja” alisema Kapinga
Aidha
kapinga alisema kuwa moja ya changamoto kubwa ni uhaba wa kupatikana
kwa dawa muhimu,vitendanish na vifaa tiba kulinganisha na utafiti wa
mwaka 2012 ulifanywa na taasisi ya afya ya Ifakarana kugundua kuwa
asilimia 41 ya dawa muhimu zinahitajika kwa kiasi kikubwa.
Kwa
upande wake afisa mchechemzi wa mradi Abrahm Kimuli aliwataka watumishi
wa sekta ya afya kuzibaini changamoto zinazowakabili na kuzitafutia
ufumbuzi kushirikiana na serikali panoja na sekta binafsi.
“Unajua
kweli kuna changamoto nyingi ambazo zinawakabili hivyo ni lazima muwe
wabunifu kuzitafutia ufumbuzi lakini kwenye hizi sekta binafsi kuwa
wasomi wengi ambao wanaweza kutoa ushauri mzuri wa kutatua changamoto
zilizopo” alisema Kimuli
Kimuli
alisema kuwa wananchi wamekuwa na uelewa wa maswala ya afya kutokana na
elimu waliopata katika mradi wa uhamasishaji wananchi kushiriki katika
masuala ya afya katika kuangalia vipaumbele vya bajeti uliokuwa
ukitekelezwa katika Mikoa ya Iringa pamoja na Dodoma.
Alisema
kuwa wananchi mradi huo katika utekezwaji wake katika Halmashauri ya
Iringa pamoja na Kongwa mkoani Dodoma wananchi wamekuwa na mwamko katika
masuala ya afya ushiriki kwa kuchangia katika huduma za afya.
Kimuli
alisema kuwa mradi huo wa miaka minne umekuwa na matokeo katika wilaya
ambazo umetekelezwa kwa wananchi kuwa na mwamko katika masuala ya huduma
za afya kwa kuchangia hata nguvu zao pale panapobidi.
Aidha
amesema kuwa mradi huo ukiisha wanaweza kufanya katika sekta zingine
ili kuwa maendeleo ya katika masuala mbalimbali kutatuliwa.
Akizungumza
kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Abel Mgimwa
alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuahakikisha
changamoto zinatatuliwa kimkakati kulinga na bajeti wanayokuwa
wameipanga.
“Ukiangalia
bajeti ya mwaka wa fedha mwaka huu imepanda hivyo ni dalili njema za
kuanza kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikidumu kwa miaka mingi na
kuwaomba wananchi na viongozi kuwa na subira katika kipindi hiki cha
utatuzi wa changamoto hizo” alisema Mgimwa
Mgimwa
aliwapongeza TACOSODE kwa mchango wao katika sekta ya afya ambayo
imekuwa na changamoto nyingi hivyo sio rahisi kwa serikali kutatua kwa
haraka hivyo.
Mkurugenzi
wa Miradi wa Tacosode, Theofrida Kapinga akizungumza jambo wakati wa
semina iliyofanyika katika ukumbi wa valentine mkoani Iringa
Afisa mchechemzi wa mradi Abrahm Kimuli akiendelea kutoa elimu kwa wanasemina walikuwa wamehudhuria katika ukumbi wa valentine
Baadhi
ya washiriki wakiwa kwenye mijadala ya sekta ya afya na jinsi gani
wanaweza kutatua changamoto zinazoweza kuikoa sekta ya afya hapa nchini
No comments:
Post a Comment