Katika
kuelekea kumbukumbu ya miaka Kumi na Minane ya Kifo cha Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere, Kituo cha Uhuru FM kupitia Kampeni yake ya Gusa
Maisha Yao, kimefanikiwa Kugusa Maisha ya baadhi ya Watanzania wenye
uhitaji kwa kutoa misaada ya Vyakula na vitu mbalimbali.
Tangu kuanza kwa Kampeni ya Gusa Maisha Yao, Kituo cha Uhuru FM
kimetembelea Vituo vyenye uhitaji wa Faraja, ambapo kimetoa msaada wa
vitu vikiwemo Vyakula katika Kituo cha Watoto Yatima-Chakuwama, na Kituo
cha Tumaini la Maisha cha Watoto wenye Maradhi ya Saratani kilichopo
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Misaada hiyo iliyotolewa na Wasikilizaji pamoja na wadau mbalimbali
imepelekwa pia katika Kituo cha Vijana walioathirika na Dawa za
Kulevya, Soba House kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam.
Kesho, Alhamis, Wafanyakazi wa Uhuru FM, kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali watajitolea kutoa Damu katika zoezi litakalofanyika kwenye
Viwanja vya Jengo la CCM, Mkoa wa Dar es salaam, Tandika Sokoni, pamoja
na Kiwanda cha Nguo Urafiki.
Kilele cha Kampeni ya Gusa Maisha Yao awamu ya kwanza kitafanyika
Jumamosi hii katika Viwanja vya MwembeYanga, Temeke, jijini Dar es
salaam kwa kuhusisha Tamasha la Michezo na Burudani ya Muziki kutoka kwa
Wasanii mbalimbali nchini kuanzia Majira ya Asubuhi hadi Jioni.
No comments:
Post a Comment