Changamoto zinazowakumba - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday 15 November 2017

Changamoto zinazowakumba



Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeendelea kupiga marufu kwa wale wote wanaohusika kuingiza mizigo ya Magendo na Dawa za Kulevya kwa kutumia usafiri wa Majini huku juhudi na hatua mbalimbali zikiwazinaendelea kuchukuliwa kwa wale wote wanao husika na biashara hiyo haramu.


Kupitia hafla ya ufunguzi wa mkutano wa  Mabaharia  ulio fanyika leo karemjee jijini Dar es sam,ambapo mgeni rasmi katika alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ambapo amewasihi  Mabaharia na Manahodha wa Meli kushirikiana na Serikali  kuwafichua wanaoingiza mizigo ya magendo na Dawa za Kulevya kupitia ukanda wa Bahari.



RC MAKONDA amesema ushirikiano huo utasaidia kudhibiti uingizwaji wa Mizigo ya Magendo Nchini.



Amesema kazi ya Ubaharia ni kazi muhimu katika kukuza wa Uchumi wa nchi kupitia ukanda wa Bahari hivyo Mabaharia wanapaswa kuona wanalo jukumu la kuchangia Ukuaji wa Pato la Taifa.

Hata hivyo MAKONDA amewaahidi Mabaharia kuwa atamfikishia Rais MAGUFULI salam zao dhidi ya changamoto  walizoainisha ikiwemo ya ugumu wa upatikanaji wa Ajira kwa mabaharia wazawa, ugumu wa kupata Mafunzo kwenye meli, Ajira kwenye Meli za uchimbaji Mafuta na changamoto za Kisera na Sheria.



Kwa upande wake msomaji wa Risala  Bw  ALOYCE MPAZI amesema watazidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha ukanda wa Bahari unakuwa moja ya nyanja zinazohusika kuchochea ukuaji wa Biashara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here