Jeshi la Polisi laagizwa kuwatia mbaroni wanasheria hawa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday 14 November 2017

Jeshi la Polisi laagizwa kuwatia mbaroni wanasheria hawa


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuwakamata baadhi ya maafisa ardhi na baadhi ya wanasheria ambao wamehusika katika uuzaji wa shamba kiasi cha Hekta mbili na nusu mali ya Madina Omary Mkazi wa Bagamoyo mkoani Pwani.

Mhe Lukuvi ametoa kauli hiyo akiwa ofisi kwake mkoani Dodoma mbele ya waandishi wa habari wakati akimrejeshea mama huyo ardhi yake huku akiwataka maafisa ardhi na wanasheria kufuata taratibu zote za uuzaji wa ardhi wakati wa kuuza.

Mhe Lukuvi amesema uuzaji wa shamba hilo ulikiuka taratibu za uuzaji wa eneo hilo ikiwemo kuwepo kwa sahihi za kufoji za wahusika wa shamba hilo huku mawikili waliofanya hivyo wakijua kuwa hilo ni kosa kisheria.

Kwa upande wake mama huyo Madina Omary amemshukuru Mhe Waziri Lukuvu kwa kumsaidia kupata ardhi hiyo ambayo alikua amedhulumiwa kwa zaidi ya miaka kumi kutoka kwa matepeli ambao alikua akishindana nao mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here