Mnada wa majengo ya Lugumi kurudiwa tena
-
KAMPUNI ya Udalali ya YONO Auction Mart
Ltd inatarajia kurudia mnada upya wa kuuza majengo ya Mfanyabiashara
Said Lugumi ili kufidia deni la Serikali,ambapo Mnada huo unarudiwa upya
baada kufanyika Mara mbili bila kufikia bei elekezi Wateja ambapo kila
mteja alifika na bei yake.
-
-
Mapema leo hii, akizungumza na waandishi
wa habari Jijini Dar as Salaam ,Mkurugenzi wa Kampuni ya YONO
Scholastika Kevela , amesema mnada huo ulifanyika kwa Mara ya TATU
ulihusisha nyumba iliyopo Mbweni JKT wilayani Kinondoni na nyingine
Upanga Wilayani Ilala.
-
-
Kevela amesema kabla kuanza kwa mnada
huo shart la kwanza waliloweka kila mteja anasajiliwa katika daftari
maalum kisha kulipa fedha taslimu sh.milioni mbili.
-
-
"Nyumba ya Mbweni JKT walijitkeza
wateja watatu na bei ya mwisho waliofika ni sh.milioni 510 na nyumba
ya Upanga walijitokeza Wateja wafanyabiashara ambao walifikia bei ya
sh, milioni 650 kiwango cha bei elekezi akijafika" amesema Kevela.
-
-
Kevela amesema kuwa, viwango hivyo vyote
ambavyo wamefika Wateja havilingani na bei ambayo Serikali wamepanga
hivyo mnada utafanyika tena mpaka sasa bado kuuzwa, huku akikataa
kuviweka wazi viwango vilivyofikiwa na wateja n kudai kua kufanya hivyo
ni ouvunja sheria za mnada.
-
-
Aidha amesema kuwa, mnada huo unaofanywa
na kampuni ya YONO kwa idhini ya Serikali ambayo ilipewa jukumu na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufidia deni la Serikali la sh
.bilioni 14 .
-
-
Awali minada iliyopita Ulifanyika
Septemba 9 mwaka huu ambapo kampuni hiyo ilifanikiwa kuuza nyumba ya
Upanga kwa sh .milioni 700 hata hivyo Serikali haikuridhika na bei hiyo
na kuamua kufanya tathimini upya ili iuzwe tena.
-
-
Pia mnada wa pili ulifanyika novemba 9
mwaka huu na Dkt. shika alifanikiwa kununua nyumba zote kwa gharama ya
sh. Bilioni 3.2 nyumba ya kwanza ya .mbweni JKT kitalu Namba 57,yenye
ukubwa wa mita za mraba 1,500 iliuzwa kwa sh,bilioni 1.1 iliyofuata
kitalu Namba 47 yenye mita za mraba 1,500 iliuzwa kwa sh.milioni 900
Nyumba ya upanga iliyopo kitalu Namba 701 yenye ukubwa wa mita za mraba
400 iliuzwa kwa sh. milioni 1.2 hata hivyo Dtk. Shika alishindwa
kulipa asilimia 25 ya fedha zote ambazo ni sh. milioni 800 hatua
iliyosababisha akamatwe na kuwekwa ndani.
-
-
Amewema kuwa kwa sasa wanajipanga tena
kwa ushirikiano na TRA wawatoa taarifa rasmi siku ya kurudia kununua
majengo hayo ya Mfanyabiashara Said Lugumi.
No comments:
Post a Comment