Rais Magufuli "Tuyapigie makelele mambo maovu - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 12 December 2017

Rais Magufuli "Tuyapigie makelele mambo maovu

Rais John Pombe  Magufuli leo Disemba 12, 2017 amewataka Watanzania pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupiga kelele kwa mambo mabaya ambayo yanaendelea nchini ili yaweze kufanyiwa kazi.




Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo na kuwataka viongozi na wajumbe hao wa Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kuwa anategemea kuona Jumuiya hiyo inaanza kupiga kelele kwa mambo mbalimbali mabaya hata kuikosoa Serikali pale inapofanya mambo tofauti. 

"Niwaombe Jumuiya ya wazazi kila kinachotokea ambacho kinakwenda tofauti na maadili ya Kitanzania hata kama tunashindwa kuchukua hatua tupige kelele, kelele zetu watu watazisikia lakini na Mungu atazisikia tufike mahali tujue maisha yetu ni ya muda hapa duniani lakini tunatakiwa tuishi katika maisha yanayomfurahisha Mungu. Ninazungumza hili kwa uchungu kwa sababu Jumuiya ya wazazi ipo ila sina kumbukumbuku kama nimewahi kusikia mahali popote mkikemea haya" alisema Rais Magufuli 
Mbali na hilo Rais Magufuli aliendelea kuwakumbusha wajumbe na viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM kuwa wanawajibu mkubwa wa kuikemea serikali ya awamu ya tano

No comments:

Post a Comment