Sanchez ndani ya Man United na Henrikh Mkhitaryan akitua the Gunners - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Sunday, 21 January 2018

Sanchez ndani ya Man United na Henrikh Mkhitaryan akitua the Gunners

Alexis Sanchez.

Alexis Sanchez anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya muda wowote kuanzia sasa ndani ya Jiji la Manchester ili kukamilisha dili lake la kujiunga na Manchester United.

Vipimo hivyo vitafanyika kwenye viwanja vya mazoezi ya Carrington ili kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo akitokea Arsenal.

Wakati huohuo, winga wa United, Henrikh Mkhitaryan naye ameonekana mitaa ya London ikielezwa kuwa anaenda kukamilisha dili la kuhamia Arsenal kwa kubadilishana na Sanchez.

Arsenal inamshusha Mkhitaryan wakati ambapo pia inamuwania straika wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang kwa ada ya pauni milioni 44 licha ya kuwa Dortmund umegoma kumuuza.

Mkhitaryan alikuwa akiongozana na wakala wake, Mino Raiola ambaye ndiye anayesimamia dili hilo, hivyo muda wowote kuanzai sasa kila kitu kitakamilika na kitatangazwa.
Sanchez ndani ya Man United  na  Henrikh Mkhitaryan akitua the Gunners

No comments:

Post a Comment