Vanessa Mdee aungana na mastaa maarufu duniani wanaomiliki majukwaa ya mtandaoni

- Vee Money App katika kilele cha maendeleo ya mziki Afrika na dunia nzima
- Vanessa Mdee anaungana na mastaa maarufu duniani ambao wanamiliki ‘majukwaa ya mtandaoni’ ya kuwasiliana na mashabiki wao
- Je
unafahamu kitu gani kinachowafananisha Taylor Swift, Ciara, na Vanessa
Mdee? Naam, pamoja na kwamba wote ni wasanii wenye sauti nzuri na vipaji
vikubwa, wote watatu wanamiliki majukwaa ‘app’ za kuwasiliana na
mashabiki wao mtandaoni.
- Hii ni njia mpya inayotumiwa na wasanii
wakubwa ambao wana mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii kama
Facebook na Instagram, ukweli ni kwamba pamoja na mitandao hiyo mikubwa
ya kijamii kutengeneza mabilioni ya dola kila mwaka wasanii hawapati
mapato ya moja kwa moja kutokana na biashara hiyo.
- Sababu
nyingine kubwa ambayo inawafanya wasanii kama Kim Kardashian kuwa na
majukwaa yao mtandaoni ‘app’ ni kwa sababu hawamiliki mashabiki wao wa
mtandaoni ila mitandao ya kijamii ndiyo ina haki juu ya watu
wanaoitumia, hii inamaanisha msanii mkubwa akifungiwa akaunti yake ya
Facebook au Instagram anaweza kukosa njia ya kuwasiliana na mashabiki
wake (Rob Kardashian ni mfano halisi).
- Pamoja na ukweli kwamba
majukwaa‘app’ pia zinaruhusu wasanii maarufu kuuza bidhaa mbalimbali na
tiketi kwenye simu za mkononi lakini cha muhimu zaidi, inasaidia wasanii
kufaidika kutokana na makampuni makubwa kutangaza kupitia majukwaa
yao.
- Kama ilivyonukuliwa kwenye mtandao maarufu wa FORBES, tangu
Juni 2014 Kim Kardashian ameingiza mapato ya zaidi ya dola za
kimarekani milioni 200. Hiyo si pesa ndogo na ni hivyo ni rahisi
kuwaelewa wasanii kama Taylor Swift, Ciara, na mwanadada anayeitikisa
Afrika Mashariki, Vanessa Mdee ambao wote wamezindua majukwaa yao ili
kukamata fursa hiyo katika mazingira ya sasa yaliyojaa maendeleo makubwa
ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
- Vanessa Mdee amechukua
fursa hii kwa kuzindua Vee Money App mwezi Januari mwaka huu. Vee Money
App, ambayo ilitengenezwa na kampuni ya teknolojia ya Marekani ya
Converge Media, imepokelewa na inaendelea kufanya vizuri kwenye soko.
- Pamoja
na kutoa maudhui ya kipekee kwa mashabiki wake, Vee Money App pia ni
jukwaa kwa watangazaji ambao wanataka kuwafikia mashabiki halisi wa
Vanessa. Hapo awali, makampuni walipotaka kutangaza bidhaa zao kwa
mashabiki wa Vanessa waliingia mikataba moja kwa moja na Facebook au
Instagram (ambao ndio wana taarifa za mashabiki) bila kumhusisha Vanessa
mwenyewe. Uwepo wa Vee Money App unamfanya sasa Vanessa kuwa mstari wa
mbele katika masuala yote yanayohusiana na matangazo kwa mashabiki wake
hivyo watangazaji sasa wanaweza kuwasiliana na kuingia mikataba moja kwa
moja na yeye binafsi.
- Mdee bado hajaacha mitandao ya kijamii
kama Instagram na Twitter, hata hivyo, maamuzi yake ya kuzindua jukwaa
lake la kuwasiliana na mashabiki kwa njia ya mtandao ni jambo la ujasiri
linalompa mwelekeo mzuri katika sekta ya mziki kama inavyoonekana kwa
Taylor Swift na Ciara. Kwa Mdee ‘Vee Money App’ ni maendeleo ya asili
katika ukuaji wake kwa ujumla katika sekta ya mziki.
- ‘Kwa kadri
ninavyoendelea kuwa katika mziki nimetambua kwamba umiliki wa kazi zako
ni muhimu sana; kuanzia kumiliki mziki wako, mashabiki wako, na majukwaa
yako ya mtandaoni na kama hutafanya hivyo mtu mwingine atakusaidia’
alisema Mdee.
- Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Biashara
wa Converge Media, Nick Brunelle, umiliki wa wasanii ndio sababu ya
uwepo wa kampuni hiyo. "Tulitaka kujenga mazingira ambapo wasanii kama
Vanessa wanaweza kuwa na umiliki si tu katika mapato ya matangazo lakini
pia umiliki katika taarifa na habari zinazohusiana na majukwaa yao"
alisema Brunelle.
- Maana yake ni kwamba tofauti na majukwaa
mengine ya mitandao ya kijamii, Vanessa anamiliki habari zote
zinazozalishwa na Vee Money App na ana udhibiti wa taarifa hizo na namna
zinavyotumiwa. "Vanessa hakika ameyapokea mabadiliko mapema hasa kwa
Afrika," aliongeza. "Ameona wazi mziki unapoelekea kimataifa na yeye
amefuata mkondo huo na kuwa kinara barani Afrika"
- Kwa sasa jukwaa
la Vanessa Mdee, Vee Money App, inapatikana bure kupitia ‘Apple App
store’ na ‘Google play store’ (Kama vile kwa Taylor Swift na Ciara
apps) . Wakati utaamua namna wasanii wanaomiliki majukwaa yao
watavyokuwa wamepiga hatua huko mbeleni lakini kwa hakika kuna ongezeko
kubwa la mashabiki wanaotamani kuwa karibu zaidi na wasanii wanaopenda
kuliko ilivyo sasa katika mitandao ya kijamii. Na Mdee ameamua kuwa
kinara katika kutimiza kiu ya mashabiki wake
No comments:
Post a Comment