Umoja
wa Wanafunzi waliomaliza Shule ya Msingi Bunge mwaka 1997 iliyopo Ilala
Jijini Dar es Salaam wametoa msaada wa viti 20 kwa shule hivyo ambayo
vitatumiwa na walimu ambao wanafundisha katika shule hiyo. Akizungumza
kuhusu msaada huo, Mwenyekiti wa umoja huo, Bernard Chezue alisema
msaada huo ni sehemu ya shukani yao kwa shule hiyo kwa kuwapatia eleimu
ambayo imewasaidia kimaisha mpaka sasa wakiwa na mafanikio. Alisema
wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kuisaidia shule hiyo ili iwe na
mwonekano mzuri jambo ambalo litachochea wanafunzi wa shule hiyo kusoma
kwa bidii.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza
mwaka 1997, Bernard Chezue akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi viti
20 kwa uongozi wa shule ya Bunge.
"Tumekabidhi
vitu hivi sabau tunaona tuna umuhimu wa kusaidia kwa sababu tumsoma
hapa na sisi tumekuwa na mafanikio kwa kupitia shule hii, tumekuja kutoa
shukrani kwa waliu wetu na shule kw ujumla, "Huu ni mwanzo tu tutaumika
nafasi yetu kutoa misaada zaidi na zaidi kwa namna Mungu anavyotujalia
maana kuja kupata rangi, kubadilisha madarasa na hata baadae kuja kutoa
zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri," alisema Chezue. Pia Chezue
aliwataka watu wengine ambao walisoma katika shule hiyo kuungana kwa
pamoja na kusaidia mahitaji mbalimbali ambayo yanahitajika shuleni
hapo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi akitoa neno la
shukrani kwa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na
kumaliza mwaka 1997 kwa kutoa msaada wa viti 20 kwa shule hiyo.
Nae
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi aliwashukuru
wanafunzi hao kwa kutambua kuwa bila shule hiyo yanawezekana wasingekuwa
na mafnikio hayo lakini pia kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo wa
kuisaidia kwa mahitaji mbalimbali.
"Nimefarijika
sana na wanafunzi waliomaliza mwaka 1997 kutuletea msaada, kwamba
wametambua mwalimu ni hazina na mafinikio waliyoyapata yametokana na
mwalimu na wameona ni vyema wawasaidie wadogo zao ili na wao wafanikiwe
kama wao walivyofanikiwa, "Tunaamini watakuja tena kufanya vitu vikubwa
sana sababu msingi waliopata katika maisha yao walipata katika Shule ya
Msingi Bunge hivyo tunaamini wameamini mafanikio yao yametokana na shule
hii," alisema Mfalingundi.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza
mwaka 1997, Bernard Chezue akimkabidhi kiti Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi. Umoja huo umetoa msaada wa viti 20
katika shule hiyo.
Wanachama
wa Umoja wa Wanafunzi ambao walisoma Shule ya Msingi Bunge na kumaliza
mwaka 1997 wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya bunge.
No comments:
Post a Comment