Aipongeza Taasisi ya Uongozi kuwaandaa watumishi wa Serikali kuwa uongozi wazuri
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
George Mkuchika amewataka Jeshi la Polisi kuwa mstari wa mbele katika
kukomesha vitendo vya rushwa huku akisisitiza kutekeleza majukumu yao
kwa misingi ya utawala bora.
Mkuchika ametoa kauli hiyo jana
jioni jijini Dar es Salaam kwa maofisa wa Jeshi la Polisi 32 kutoka
mikoa mbalimbali nchini ambao wamehitimu mafunzo ya Stashahada ya
Uzalimi ya Uongozi kutoka Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute).
Mafahali
hayo ni ya kwanza kutolewa na taasisi hiyo ambayo wameshirikiana na
Chuo cha Aalto cha nchini Finland na hivyo kufanya mafunzo hayo
kutambulika na kukubalika kimataifa kuhusu masuala ya uongozi.
Hivyo
akizungumza na maofisa hao pamoja na wageni wengine waalikwa ,Mkuchika
amewapongeza wahitimu hao lakini awakata kuwa mstari wa mbele wao
pamoja na jeshi la polisi kwa ujumla wake kupambana na komesha rushwa.
Amesema
katika mataifa mbalimbali maeneo ambayo rushwa inaangaliwa sana ni
katika Mahakama na Polisi .Hivyo ni vema polisi nchini wakawa mstari wa
mbele kukomesha rushwa.
"Mataifa mengi yanapimwa katika mambo ya
kupambana na rushwa pamoja na kuangalia maeneo mengine pia wanaangalia
na Jeshi la Polisi.Na kwa bahati mbaya kwenye nchi nyingi baadhi ya
polisi wamekuwa wakituhimiwa kujihusisha na rushwa, hivyo ni vema
waliopata mafunzo hayo ya uongozi wakawa mabalozi wa kukemea rushwa
nchini,"amesema Mkuchika.
Amefafnua wizara anayaoingoza Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), ipo chini yake na ndio maana
amezungumzia suala la kupambana na rushwa na kueleza hata akipata
mualiko kwenye sherehe za harusi bado atazungumzia umuhimu wa kukomeshwa
rushwa nchini kwani ni adui wa haki.
Amewataka Polisi nchini
kutekeleza majukumu yao kwa kuheshimu misingi ya utawala wa bora na
kusisitiza kuwa taaswira ya nchi wakati mwingine inapimwa kwa kulitazama
jeshi hilo.Hivyo waliopata mafunzo hayo ya uongozi watakuwa washauri
wazuri kwa maofisa wengine wa Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu
yao na mafunzo hayo yawe chache katika maeneo ya kazi.
Mkuchika
amesema anatambua gharama ya mafunzo hayo, hivyo wahitimu wajue wanalo
deni kubwa la kuwatumikia Watanzania na kuthibitisha kwa vitendo wameiva
kwenye mafunzo ya uongozi ambayo yamewajenga katika kutoa maamuzi ya
kimakakati.Kuhusu Taasisi ya Uongozi, Mkuchicha amesema anatambua kazi
kubwai inayofanywa na taasisi hiyo chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu wake
Profesa Joseph Semboja ya kupika na kuandaa watumishi wa umma katika
masuala ya uongozi nchini.
"Kutokana na umuhimu wenu ndani ya
nchi yetu, nilikuwa Dodoma na nilichofanya ni kuwaombea bajeti kwa ajili
ya kuendesha shughuli zenu.Niwaambie bajeti ile imepitishwa.Serikali
tunatambua mchango wenu katika kuandaa watumishi kuwa viongozi
wazuri."Nikiri wapo ambao wamezaliwa na kipaji cha uongozi lakini ukweli
uko palepale tafiti zinaonesha uongozi unasomewa na kujifunza kutoka
kwa wengine kupitia vitabu, majarida na kukaa darasani,"amesema
Mkuchika.
Amewapongeza wahitimu hao pamoja na wale ambao
wamejiunga katika taasisi hiyo kwa ajili ya mafunzo hayo ambayo
yanatarajia kuanza hivi karibuni na miongoni mwa waliomba mafunzo hayo
yupo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
Kwa upande Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja amesema
mahafali hayo ni kwanza kwa Stashahada ya Uzalimi ya Uongozi ambayo
taasisi hiyo wameianzisha.Stashahada ya Uzamili ya Uongozi ni programu
ya mafunzo ya utawala yanaendeshwa na taasisi hiyo pamoja na Chuo Kikuu
cha Kifini cha Aalto cha Mafunzo ya utawala.
Programu hiyo
inalenga hasa kutoa mbinu na nyenzo za uongozi kwa viongozi wa Serikali
wa ngazi za juu,nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla ili kufikia
maendeleo endelevu.Stashahada hiyo ina moduli 10 na ni ya kipindi cha
mwaka mmoja.Kundi la kwanza la washiriki wa Stashahada hiyo wamehitimu
jana na walianza mafunzo Aprili mwaka 2017.
Ambapo Profesa
Semboja amefafanua mafunzo hayo yanajenga uwezo wa kiongozi katika
kusimamia masuala mbalimbali na hasa kufikiri kimkakati na kutenda na
kuamua kwa njia iliyosahihi."Mafunzo ya Stashahada ya Uzamili inatoa
nafasi ya kumuandaa mhitimu na kuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza na
kuandaa viongozu wenye uwezo wa kufikiria vema.
" Pia mhitimu wa
mafunzo haya anaweza kujiendelea kielimu katika Chuo cha Aalto ambacho
ni moja chuo kikubwa nchini Finland,"amesema Profesa Semboja.Amesema
changamoto kubwa ya Staahahada ya Uzamili ya uongozi ni gharana kubwa na
kufafanua wahitimu wapatao 32 wamehitimu na anaamini watatoa mchango
mkubwa katika maeneo yao ya kazi.
Profesa Semboja amempongeza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kwa uamuzi wake wa kuomba kujiunga
na taasisi hiyo ili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment