
Chumi amesema hayo wakati akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni.'Mhe Mwenyekiti, serikali imekiri kuwa usambazaji wa mbolea ulikuwa 64% mana yake ni kuwa 36% ya wakulima hawakupata mbolea'
'Sio
hivyo tu, hata hiyo 64% hawakupata mbolea kwa wakati, sio haki kabisa,
mkulima wa Itimbo, Kitelewasi, Isalavanu apelekewe mbolea ya kupandia
mwezi February wakati uandalizi wa mashamba unaanza mapema Oktoba.'
Kuzuia kuuza ziada ya mazao ni kuwaonea wakulima Akizungumzia
wakulima kuuza mazao yao,nje ya nchi, Chumi alisema kuna ziada ya tani
2.6milioni ya chakula, lakini Hifadhi ya Taifa ya Chakula imenunua tani
26,000(elfu ishirini na sita tu), afu mkulima anazuiwa kuuza mahindi
yake, jambo ambalo sio sawa.
Tunawafanya wakulima wa nchi hii kama raia daraja la pili (second citizens),mbolea
tuwacheleweshee, ziada ya mazao yao tuwafungie kuuza, hii sio sawa'
alisisitiza Mbunge huyo na kuongeza kuwa ni vizuri serikali ikaangalia
changamoto ilizokutana nazo katika usambazaji wa mbolea mwaka huu na
kuboresha mazingira ili kumsaidia mkulima kupata mbolea kwa bei nafuu,
kwa wakati na pia kuuza ziada ya mazao.
Awataka Wawekezaji Mafinga kuwajali wafanyakazi
Akizungumzia
haki za wafanyakazi, Chumi alisema kuwa anapongeza jitihada za Rais
John Magufuli kuvutia wawekezaji, lakini akaitaka Wizara ya Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi na Ajira kutupia jicho haki za wafanyakazi kwenye
Viwanda vya Mafinga.
Uchumi wa
Viwanda lazima uendane na welfare ya wafanyakazi, itakuwa haina mana
kuwa na viwanda lakini hali za wafanyakazi zinakuwa duni, lazima walipwe
vizuri, waangaliwe huduma za afya na kulipiwa nssf , alisisitiza Mbunge
huyo.
Akifafanua, alisema sio haki mfanyakazi anatoka Changarawe, anatembea mpaka kilometa nne kwenda kazini, sio haki.ni
hatari sana, unakuta mama anaamka saa kumi alfajiri kuwai kazini ambako
nako halipwi vizuri, nikuombe mama Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu) na kaka yangu Mavunde (Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Vijana) nadhani ni mdogo wangu kufika
Mafinga na kutoa maelekezo.
Apongeza Mhe Rais kukutana na Wafanyabiashara, ashauri akutane nao Kisekta
Tumeona
ambavyo Jumuiya ya wafanyabiashara walieleza kero zao na Mhe. Rais na
Rais akaagiza Mawaziri wazifanyie kazi, lakini nimuombe Mhe Rais akutane
na Wafanyabiashara kisekta mana siku ile wote tuliona muda ulikuwa
mdogo kwa mfano anaweza kukutana na sekta ya usafirishaji.
Akizungumza
baadae na Mwandishi wetu, Chumi alisema kuwa mazingira wanayofanyia
kazi wafanyakazi kwenye Viwanda vya Mafinga hayaridhishi na
wanapolalamika kwa baadhi ya viongozi taarifa hurejeshwa kwa wenye
viwanda kwa siri na matokeo yake mlalamikaji hutafutiwa visa na
kufukuzwa kazi.
No comments:
Post a Comment