Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Mb.)
akihutubia kwenye Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani, unaowakutanisha
wadau mbalimbali wanao simamia na kutengeneza vifaa na miundombinu
mbalimbali ya Tehama. Mkutano huo unatarajia kuangalia namna mbalimbali
za kupambana na matumizi ya Tehama yanayochafua mazingira; umehudhuriwa
na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akiwemo Waziri wa Ujenzi,
Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Dkt. Sira Ubwa (Mb.), Katibu Mkuu
(Mawasiliano) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Maria
Sasabo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi, Mkurugenzi wa ITU
(International Telecomunication Union), Dkt. Chaesub Lee, Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Kilaba. Mkutono huo
unafanyika katika Hoteli ya Sea Clif Mangapwani, Zanzibar kuanzia tarehe
9-12, Aprili 2018.
Waziri
wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa,
akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo visiwani Zanzibar na kuelezea
faida ya mkutano kufanyikia Unguja. Alisema kwa mazingira ya sasa,
changamoto iliyopo mbele yetu ni kushirikiana kwa pamoja ili kuziepusha
nchi zetu na uharibifu utokanao na matumizi ya vifaa chakavu vya
kielektroniki. Mhe. Dkt. Sira alitumia fursa hiyo kuwapongeza kwa
mjadala muhimu utakaoendelea wa utunzaji wa mazingira na kuwasihi
wasiache kutembelea vivutio vya asilia vilivyopo visiwani humo.
Mkurugenzi
wa International Telecommunication Union (ITU) Dkt. Lee akizungumza
kuhusu mjadala na maazimio ya mkutano huo muhimu wa kimataifa wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Wiki ya Kijani.
(Juu
na Chini) Sehemu ya wajumbe na washiriki mbalimbali wa mkutano huo
wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wakati wa ufunguzi wa
mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Balozi Mwinyi akielezea jambo huku Dkt. Ubwa na Dkt. Sasabo wakimsikiliza.
Picha
ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Wiki
ya Kijani, unaoendelea kwenye Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar tarehe 9-12,
Aprili, 2018
No comments:
Post a Comment