YANGA KUANZA NA IHEFU AU TUKUYU STARS, AZAM NA MADINI AU STAND BABATI, SIMBA SC NA MASHUJAA KOMBE LA TF - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 12 December 2018

YANGA KUANZA NA IHEFU AU TUKUYU STARS, AZAM NA MADINI AU STAND BABATI, SIMBA SC NA MASHUJAA KOMBE LA TF

RATIBA KAMILI AZAM SPORTS FEDERATION CUP 
Namungo FC v Sahare All Stars/Deportivo
Geita Electrict/Kamuyange v Kagera Sugar
Mtibwa Sugar v Kiluvya United
Lipuli FC v Laela FC/Mitumba FC  
Stand United v Ashanti United
Changanyikeni/Barger FC v Coastal Union
Reha FC v Zakhem/Mkamba Rangers
Maji Maji FC v Toto Africans/Gipco
Boma FC v Njombe Mji FC
Pan African /Villa Squad v Mwadui FC
Cosmopolitan v Green Warriors 
Rhino Rangers v Nyamongo FC/Bulyanhulu FC
Azam FC v Madini FC/Stand Babati
KMC v Tanzania Prisons
Kilimanjaro Forest /Kilimanjaro Heroes v Polisi Tanzania
Moro Kids/Maji Maji Rangers v Mbeya Kwanza 
Geita Gold FC v Biashara United 
Ruvu Shooting v Mucoba FC/Might Elephant 
Yanga SC v Ihefu FC/Tukuyu Stars
Singida United v Arusha FC 
Sharp Striker/Usalama v Friends Rangers 
Dodoma FC v Kasulu Stars/Home Boys
Mufindi United v Alliance FC
Mbeya City v Mgambo Shooting 
African Lyon v Arusha United 
Simba SC v Mashujaa FC (Kigoma) 
La Familia/Area C v Mawenzi Market 
Mbao FC v Dar City 
Stand Dortmund/Milambo FC v JKT Tanzania  
Mtwivila/Livingston v Pamba FC 
Ndanda FC v Trans Camp
Mnale FC v Kitayose/African Sports
(Mechi zitachezwa kuanzia Desemba 21 hadi 24, 2018)

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
VIGOGO, Azam, Simba na Yanga wote wataanzia nyumbani hatua ya 64 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ijulikanayo kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Hiyo ni baada ya droo ya raundi ya tatu ya michuano hiyo, iliyofanyika leo makao makuu ya Azam TV, hapa Tabata, Dar es Salaam ikishuhudiwa KMC NA Tanzania Prisons kuibuka mchezo pekee utakaokutanisha wapinzani wa Ligi Kuu watupu.
Azam FC watakuwa wenyeji wa ama Madini FC ya Arusha, au Stand ya Babati, Yanga SC wataikaribisha amaIhefu FC au Tukuyu Stars, zote za Mbeya na Simba SC watawaalika Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma.
Mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wao wataanza na Mtibwa Sugar na Kiluvya United ya Pwani Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, wakati washindi wa pili Singida United wataanzia nyumbani pia Uwanja wa Namfua mkoani Singida dhidi ya Arusha FC. 
Mechi zitachezwa wikiendi ijayo kuanzia Desemba 21 hadi 24 na hii moja kwa moja inamaanisha mechi itachezwa kabla au baada ya mchezo wa marudiano wa Simba na Nkana Desemba 23 Dar es Salaam, lakini mabingwa wa Tanzania Bara wanajivunia kikosi kipana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here