![]() |
| Picha ya Maktaba |
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) hii leo imefunga machinjio ndogo ya Msalato na kupiga faini kwa kosa la kukithiri kwa uchafu.
Hatua hiyo imefikiwa leo mara baada ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo na kujionea Mazingira yasiyoridhisha kwa usalama wa afya za binadamu.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mussa Sima amesema lazima hatua kali zichukuliwe kwa manufaa ya afya za walaji.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge Kanali Mstaafu Masoud Ally Khamis alisema endapo NEMC wasingechukua hatua hiyo basi wao wangeyafungia machinjio hayo.
Baadhi ya wananchi wanaotumia machinjio hiyo wamelalamikia hatua hiyo na kutoa lawama kwa Jiji la Dodoma kutozingatia udafi wa mazingira katika eneo hilo licha ya kua wanatoa ushuru.

No comments:
Post a Comment