Auawa kwa tuhuma za kuvunja Nyumba - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 15 November 2019

Auawa kwa tuhuma za kuvunja Nyumba




Wananchi wenye hasira kali katika mtaa wa Majengo  halmashauri ya mji wa Makambako  mkoani Njombe wamemuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Isega Wilson Mozya mkazi wa mkoa wa Songwe kwa tuhuma za kuvunja nyumba ya Bwan. Roden Mandela kwa lengo la kutaka kuiba.
Jeshi la Polisi Mkoani humo kupitia Kamanda Hammis Issa limesema limefika eneo la tukio na kukuta marehemu huyo akiwa tayari ameuawa huku akiwa na siraha aina ya chinese pistol yenye namba 13034032 ikiwa na risasi saba pamoja na vifaa vya kuvunjia milango .
“Na hizi bastola zinatumiwa na majeshi yetu na mpaka saizi hii bastola tunaifanyia uchunguzi ni ya sehemu gani katika majeshi yetu ya hapa Tanzania”anasema Kamanda
Aidha amesema wamemkuta marehemu huyo akiwa na vifaa mbali mbali ikiwemo bisi bisi pamoja na vifaa vingine anavyoweza kufanyia uhalifu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here