CCM yavunja ngome ya CHADEMA, Buchosa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 5 November 2019

CCM yavunja ngome ya CHADEMA, Buchosa



Wanachama 18 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Bulyaheke Matias Ngoso wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM

Wameeleza sababu za kuhama CHADEMA na kujiunga CCM ni kutokana na Serikali ya Awamu ya Tano inavyowahudumia wananchi kwa kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa vitendo na hafra ya kuwapokea imefanyika kitongoji Cha Zilagula kata ya Bulyaheke.

Mmoja wa wanachama wa CHADEMA aliyeshika nyazifa nyingi za uongozi kwenye chama hicho Matias Ngoso alisema walipokuwa chadema walikuwa wanaaminishwa kutokuamini ukweli na kuaminishwa uongo kuwa ukweli.

Alisema katika chama hicho aliwahi kushika nyadhifa nyingi tangu ajiunge na Chadema mwaka 2009, ikiwemo ujumbe wa mkutano kuu Jimbo la Buchosa, aligombea udiwani mwaka 2010 ,aliwahi kuwa mkuu wa mafunzo ya red briged ya chama hicho .

Wakati akihama chama hicho alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Bulyaheke na Kampeni Meneja wa wagombea ubunge, mwenyekiti wa Kijiji na Vitongoji ,kuhama kwake Chadema kumeivunja nguvu na kuizika Jimbo la Buchosa na Sengerema kwa ujumla.

Baadhi ya wanachama  wengine waliorudisha kadi Magreti Lufungulo alisema kuwa  kurudisha kwake CCM kumemuondolea matatizo aliyokuwa nayo alipokuwa Chadema ya kupinga kila Jambo ambalo limefanywa na serikali hiyo CCM ndiyo mahali sahihi pa kumaliza matatizo hayo.

Akiwapokea wanachama hao Katibu wa CCM Kata ya Bulyaheke Fredriki Kondola alisema leo tumewapokea wanachama 18 akiwemo Aliyekuwa anatutesa  akiwa Chadema kwenye kampeni Matias Ngoso nijambo la kujivunia tutawatunza na wanatakiwa kukitumikia chama kwa moyo wa upendo.


Kondela alisema chama Cha mapinduzi CCM ndiyo chama pekee ambacho kitafanya watanzania kuwa kuwa na maisha Bora kutokana serikali ya awamu tano inavyochapa kazi na kuwajali wanachi wake.

" Tunapaswa kuwapokea na chama kitaendelea kuwachunguza hivyo nilazima wawe watulivu na waadilifu chama chetu kitaendelea kuvuna wanachama wengi,".alisema Kaondela.

Aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Zilagula kupitia Chadema miaka kumi Abushili Rashidi ambaye anawaniwa kiti hicho kwa muhura tatu alisema kuhama kwao hakujaipunguza CHADEMA nguvu ya kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mratibu wa uchaguzi kata ya Luharanyonga Kaburenge Obote pamoja na mratibu wa uchaguzi Kata ya Bulyaheke  Nundi Makeleko waliohdhuria hafla ya kuwapokea wanachama hao walisema wamechagua mahali sahihi ambapo walitakiwa kuwa hivyo.

Wanachama hao 18 waliohama CHADEMA na kujiunga na CCM alisema kuwa watakuwa waadilifu na kushirikiana ili wakikomboe kitongoji Cha Zilagula ambacho kimeongozwa na Chadema ndani ya miaka kumi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here