Fahamu kuhusu ugonjwa wa Polio kiundani zaidi - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday, 17 November 2019

Fahamu kuhusu ugonjwa wa Polio kiundani zaidi

Polio ni ugonjwa wa kuambukiza usababishwao na virusi, huathiri neva na kusababisha ulemavu.
Kutokana na taarifa za shirika la afya duniani:Polio huathiri zaidi watoto wa umri wa chini ya miaka mitanoUlemavu hutokea kwa mmoja kati ya maambukizi 200Mpaka 2013 ni nchi tatu ambazo bado kuna mlipuko wa ugonjwa huu wa kupooza Afghanistan, Pakistan na Nigeria. Ila kutokana na Taarifa kutoka wizara ya afya ya Tanzania ilipokea taarifa kutoka shirika la afya duniani kuwa kuna mlipuko katika nji jirani ya Kenya, wilaya ya Fafi.
Je ni zipi dalili za ugonjwa huu?Dalili hizi hudumu kwa kati ya siku 1 hadi 10HomaMaumivu ya kichwaKutapikaUchovuMaumivu ya shingoMaumivu ya mgongoMaumivu ya mikono na miguuMisuli kukakamaa
Je ni matatizo gani mtu huweza kupata baada ya maambukizi haya?Kupooza misuliUlemavu wa miguu
Vipimo:Virusi vya polio huweza kuonekana katika makohozi, kinyesi na maji maji ya uti wa mgongo.
MatibabuHamna matibabu ya maambukizi haya, kwahiyo ni tiba ya dalili ambayo hutolewa:KupumzikaDawa za kutuliza maumivu na kushusha homaAntibiotiki kuzuia maambukizi nyemeleziMazoezi kiasi kwaajili ya kuzuia kukakamaaNa kula chakula bora
KingaNi chanjo ya Polio ambayo hutolewa pamoja na chanjo nyingine kwa watoto baada tu ya kuzaliwa, na kurudiwa tena katika wiki ya nne, ya nane na mwisho ya kumi na mbili.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here