Jinsi ya kupika ndizi mchemsho - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

KABATA2

Wednesday, 13 November 2019

Jinsi ya kupika ndizi mchemsho

hqdefault

Ndizi ni moja ya chakula kinachopendwa sana na watu wengi, lakini kwa hapa nchini chakula hiki huongoza kwa kuliwa zaidi na watu wa kabila la Wahaya kutoka mkoa wa Kagera, Bukoba. Sasa leo katika mapishi tutaandaa ndizi mchemsho twende sote...
MAHITAJINyama roboNdizi mzuzu mbichi 5 au kulingana na ukubwa wa familia yakoVitunguu majiGiligiliani vijani kiasiVitunguu swaumuRosemary (vijani vichache)Bay (vijani kiasi)KarotiChumviOliver oil kijiko cha mezani kimojaBlack pepperChills endapo unapenda
Namna ya kuandaaMenya ndizi zako na uzioshe vizuri kwa maji safi na salama.
Katakata vitunguu maji, na karoti kwa mtindo uupendao
Jinsi ya kupikaChemsha nyama na ikiashaiva vizuri weka chumvi kiasi, bay, rosemary, black paper vyote hivi utaweka wakati nyama ikiendelea kuchemka.
Nyama ikishaiva vizuri weka vitunguu maji na vitunguu swaumu pamoja na nndizi kisha acha viive vyote kwa pamoja, lakini kabla ya kutoa weka karoti.Baada ya dakika 5 unaweza kutoa chakula motoni na kitakuwa ni tayari kimeiva na unaweza kula mchana au usiku pia.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad