Korea Kaskazini imesema leo kuwa hatua ya Marekani kuirejesha nchi hiyo kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi inahujumu matarajio ya juhudi za kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Taarifa hiyo imekuja wakati nchi hiyo ikiendeleza shinikizo kwa Marekani kuhusiana na mkwamo wa mazungumzo ya nyuklia.
Wiki iliyopita, ilifyatua makombora iliyoyataja kuwa ya kisasa ikiwa ni tukio la kwanza la jaribio la makombora kufanywa katika mwezi mmoja.
Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Korea Kaskazini imesema leo kuwa ripoti ya ugaidi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani wiki iliyopita inadhihirisha kwa mara nyingine kuwa Marekani inatekeleza sera ya uhasama kuelekea Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini imekuwa kwenye orodha mbaya ya ugaidi kwa miongo miwili baada ya majasusi wake kulaumiwa kwa ulipuaji bomu wa ndege ya Korea Kusini ambao ulisababisha vifo vya watu 115 katika mwaka wa 1987.
Iliondolewa 2008 wakati Marekani ikijaribu kuishawishi Kotrea Kaskazini kufikia makubaliano ya nyuklia.
No comments:
Post a Comment