Marekani imeanza rasmi mchakato wa kujiondoa katika makubaliano ya kihistoria ya mazingira yaliyofikiwa Paris mwaka wa 2015.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema kuwa amewasilisha barua rasmi kwa Umoja wa Mataifa.
Mchakato wa kujiondoa utachukua mwaka mmoja ili kumalizika rasmi. Taarifa ya Pompeo ilielezea kuhusu kile alichokiita "mzigo usio wa haki wa kiuchumi uliowekwa kwa wafanyakazi wa Marekani, biashara, na walipa kodi, kwa ahadi za Marekani zilizotolewa chini ya makubaliano hayo,".
Karibu mataifa 200 yalisaini mkataba huo wa mazingira ambapo kila nchi inatoa malengo yake ya kupunguza utoaji wa hewa chafu inayosababisha mabadiliko ya tabianchi.
Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa mpinzani mkubwa wa makubaliano hayo wakati alipokuwa anawania kiti cha urais, na utawala wake umekuwa ukifanya kila unaloliweza kubadilisha sheria za mazingira, ukisema zinazuwia biashara na kutoa kwa nchi nyingine nguvu ya ushindani.
No comments:
Post a Comment