Mchezo wa Kirafiki kati ya Argentina na Uruguay hatarini kufutwa - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 13 November 2019

Mchezo wa Kirafiki kati ya Argentina na Uruguay hatarini kufutwa



Mchezo wa Kirafiki kati ya Argentina na Uruguay huko Tel Aviv kuna mashaka makubwa usifanyike, baada ya Israeli kupigwa na makombora yaliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza (Palestina)
Mchezo huo umepagwa kufanyika Novemba 18 mwaka huu lakini baada ya shambulio la hivi karibuni, upo uwezekano linaweza kuahirishwa.
Michezo mingine iliyotarajiwa kufanyika nchini Israeli imefutwa na sasa mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kumshuhudia nyota wa soka Lionel Messi akirejea kwenye kikosi cha Argentina upo uwezekano ukafutwa.
Japokuwa Makombora hayo kawaida hayawezi kufikia mji mkuu wa Israeli - lakini hiyo sio sababu ya kuzuia viongozi wa Israel kuwa waangalifu.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here