Mwinyi Zahera ashangazwa na ratiba ya Ligi Kuu - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Monday, 4 November 2019

Mwinyi Zahera ashangazwa na ratiba ya Ligi Kuu


Baada ya kurejea leo akitokea Cairo, Misri ambako alikuwa na kibarua cha kuiongoza Yanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ameshangazwa na ratiba ya ligi.

Zahera ameelezwa kushangazwa baada ya kupata taarifa kuwa watakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara Ijumaa ya wiki hii dhidi ya Ndanda FC ambapo watapaswa kusafiri kwenda Mtwara.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Congo, ameeleza kuwa alikuwa hana taarifa kabisa juu ya uwepo wa mchezo huo jambo ambalo limemshangaza.

Akizungumza mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege, Zahera amezungumza akiwa anajua watakuwa na siku kadhaa za kupumzika kutokana na safari ya kutoka Misri.

Kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Pyramids FC hapo jana kimewaondoka rasmi Yanga kunako mashindano hayo na wapinzani wao wakiingia hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment