Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere siku moja baada ya kuapishwa, CAG aliyemaliza muda , Prof. Mussa Assad Juma amempa ushauri wa namna ya kuendesha ofisi.
Profesa Assad amemueleza kuwa ni vyema akawajengea uwezo watumishi waliopo kuliko kuwafanyia mabadiliko kwa haraka kwa sababu hatua hiyo inaweza kuharibu utendaji wa taasisi.
“Taasisi haitakiwi kufanyiwa mabadiliko ya haraka muhimu ni kuwajengea uwezo waliopo, kinyume na hapo unaweza kuharibu taswira.”
“Huwa naamini changes (mabadiliko) zinaweza kutokea ila zitokee katika namna ambayo zimepangwa vizuri, si mwaminifu katika mfumo wa kutoa watu wote na kuweka new team usually lazima kutakuwa na mkanganyiko and can be very expensive kwa institutions kama hizi ambazo mtu anajifunza kwa miaka mingi.

No comments:
Post a Comment