Serikali imesema inatambua umuhimu na kazi kubwa zinazofanywa na asas za kiraia AZAKI hapa nchini katika kutoa elimu na kuwajengea uelewa wananchi katika nyanja mbalimbali.
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, wakati akifungua wiki ya asasi za kiraia inayofanyika Jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri, sambamba na Kongamano la asasi za hizo ambazo zimekutana Jijini Dodoma, na kuonesha shughuri wanazozifanya katika maeneo yao.
Amesema serikali inatambua kazi kubwa zinazofanywa na asasi hizo katika kuwaongezea wananchi na viongozi uwezo katika kutimiza majukumu yao na baadhi ya asasi hizo zimekuwa zikiwajengea uwezo jamii na hasa maeneo ya vijijini.
" Sisi Kama serikali tunaona mchango mkubwa wa asasi za kiraia katika kutoa elimu na kuwajengea uwezo wananchi na viongozi hasa maeneo ya vijijini wanatusaidia Sana kuwajengea uwezo wananchi" amesema Majaliwa.
Amesema baadhi ya asasi za kiraia zimekuwa zikijishughulisha na kutoa elimu ya kuepuka na kujikinga na magonjwa mbalimbali elimu ambayo imekuwa ni msaada mkubwa kwa Jamii zetu na ni malengo ya serikali katika kutoa elimu hiyo kwa jamii.
Amesema wamewahi kufanya utafiti kwa asasi za kiraia zipatazo tisini na mbili(92) wamebaini kuwa zimekuwa zikipata fedha zaidi ya Bilioni Mia mbili hamsini, (Bilioni 250) fedha hizo ni nyingi sana ni lazima ziingie katika kufanya kazi kwa wananchi na sio kuingia kwenye semina tu.
Amewataka wajikite katika maeneo ya vijijini huko ndiko kwenye mahitaji sana, hasa msaada wa kisheria, amewataka katika majukumu yao wahakikishe wanawahimiza wananchi katika kulipa kodi ili serikali kufikia malengo yake.
Ameongeza kuwa" sisi Kama serikali tutaendelea kushirikiana na asasi za kiraia katika kutimiza majukumu yenu, na serikali itaendelea kuondoa vikwazo vyote vinavyokutana navyo katika shughuri zenu" amesema.
Kwa upande wake Rais wa Foundation for Civil Society, (FCS), Dkt Stigmata Tenga, kupitia wiki ya asasi za kiraia zinapata fulsa ya kuonesha shughuli wanazozifanya katika maeneo mbalimbali hapa nchi na kauli mbiu ya wiki hiyo ni "ubia kwa Maendeleo, ushirikiano Kama nguzo ya Maendeleo Nchini Tanzania".
Ameongeza" hapa nchini kumekuwa na ongezeko la asasi za kiraia zipo takribani elfu 6000 na zimejikita katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kujishughulisha na mambo mbalimbali katikakazi za kitaifa, mikoa, wilaya, Tarafa, kata na vijiji" amesema Dkt Stigmata.
Amesema wanashirikiana na Serikali katika majukumu yao, na kwa ushirikiano mkubwa na wanatambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika nyanja mbalimbali kutika kuwatumikia wananchi.
Ameiomba serikali katika bajeti zao waone namna ya kutenga fungu kwa ajili ya asasi za kiraia katika kuziwezesha Kama luzuku kutimiza majukumu yao na kuongeza ufanisi zaidi katika shughuli zao za kila siku kuwatumikia wananchi.
Naye Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema Wizara yake ndio msimamizi Mkuu wa shughuli zote za asasi za kiraia na kunaidara maalumu ambayo inaratibu shughuli zote za asasi za kiraia na wanashirikiana nao vyema.
Ameongeza kuwa " wanashirikiana vyema na asasi zote za kiraia na asasi nyingi zimejipambanua kufanya kazi na jamii hasa zile za chini kabisa na watu wasiojiweza, katika maswala mbalimbali Kama Afya,elimu,maji na msaada wa kisheria vitu ambavyo vinaungwa mkono na Serikali" amesema Waziri Ummy.

No comments:
Post a Comment