Serikali yafikiria likizo kwa wanaojifungua watoto njiti - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 15 November 2019

Serikali yafikiria likizo kwa wanaojifungua watoto njiti


Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema ombi la wanawake wanaojifungua watoto njiti kupewa msaada wa chakula na likizo ya miezi sita kwa wafanyakazi linahitaji mchakato wa kisheria.
Balozi Mahiga ameyasema hayo katika kongamano la wiki ya mtoto njiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dar es Salaam wakati akijibu hoja iliyotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Getrude Mongela.
Awali, akizungumza katika kongamano hilo, Mongela amesema kwakuwa wanakaa kutunza watoto katika vifua vyao kwa kipindi kirefu, wanahitaji chakula kwani kinamama hao wanawalea wakiwa hospitalini hivyo wanakuwa hawana uwezo wakutafuta.
“Si hili pekee kwa wale wanaofanya kazi kuna haja ya kuongezwa siku za maternity kutoka miezi mitatu wanataka iwe miezi sita hili linawafanya wengi wanaacha kazi kwa ajili ya kulea watoto,” amesema Mama Mongela.
Balozi Mahiga amesema ombi hilo haliwezi kujibiwa kwa sasa kwani kuna mambo ya kisheria hivyo ni suala ambalo linahitaji mashauriano ya wadau mbalimbali ikiwemo wizara ya Afya, Tamisemi na Wizara zingine.
“Kama waziri wa sheria siwezi kusimama na kusema nimelipitisha, ni suala ambalo linahitaji mashauriano, tupo wadau wengi kikubwa ni kwamba tuelewe matatizo ambayo mmeyaeleza hapa nimeyaelewa nimeyachukua,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here