Shambulizi la bomu katika kituo cha polisi Indonesia
Kituo cha polisi kimeshambuliwa kwa bomu kwenye kisiwa cha Sumatra huko Indonesia.
Kulingana na gazeti la Tempo huko Indonesia, watuhumiwa wawili walitega bomu hilo kupitia mlango wa kuingilia wa Kituo cha Polisi cha Meran.
Washambuliaji hao wanakadiriwa kuwa wamekufa kwenye eneo la tukio la mlipuko huo, wakati viongozi bado hawajatoa taarifa kamili kuhusu suala hilo.
Hatua kali za usalama zimechukuliwa katika kituo cha polisi ambapo shambulizi hilo limefanyika, na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
No comments:
Post a Comment