Wednesday, 27 November 2019
Ugonjwa Wa Kansa Ni Nini? Chanzo Cha Saratani Na Aina Za Saratani
Kama umekuwa ukisikia kuhusu ugonjwa wa kansa au saratani na ukawa unajiuliza ni nini ugonjwa huu wa kansa, pitia ukurasa huu ambamo tutatazama maana ya ugonjwa huu, chanzo chake, madhara anayoweza kupata mtu mwenye ugonjwa huu na tiba ambazo hutolewa kukabiliana na tatizo la kuumwa na ugonjwa huu wa kansa.Kansa (saratani) ni neno lililotolewa kwa kundi la magonjwa yanayosabahiana. Kuna aina tofauti zaidi ya 100 ya magonjwa yanayoitwa kansa au saratani. Katika aina zote hizi za saratani, baadhi ya seli za mwili huanza kujigawa bila kusimama na kuenea kwenye maeneo ya karibu ya mwili. Kansa huweza kuanza kwenyesehemu yo yote ya mwili. Kwa kawaida seli za mwili hujigawa na kuzalisha seli mpya kulingana na mahitaji ya mwili, seli za zamani zikiharibika au kuzeeka, seli mpya huchukua nafasi ya seli hizo.Saratani inapotokea, mpangilio huu huvurugika. Kadri uvurugikaji huu unavyozidi, seli za zamani zinaendelea kuishi badala ya kufa na seli mpya hutengenezwa bila mahitaji ya mwili. Seli hizi za ziadahuendelea kujigawa na kujenga uvimbe (tumors). Saratani za aina nyingi hujenga uvimbe isipokuwa saratani za damu, kama leukemia, ambapo ugonjwa huu huzuia ufanyakazi kazi wa kawaida wa damu kwa kusababisha kugawanyika kwa seli za damu kusiko kwa kawaida.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment